Saturday, June 20, 2015

RAMADHANI KAREEM

Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, tunawatakia ndugu zetu waislamu mfungo mwema.

Friday, June 19, 2015

KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA 2015

Ndugu Watanzania tunayo  kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuuona huu mwaka wa uchaguzi. Pia tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia Amani katika nchi yetu ya Tanzania. Japo wapo watanzania wengi wanaoishi katika shida lakini lililo kuu kwetu sisi binadamu ni Amani na Utulivu. Tukiwa katika kipindi hiki cha kuelekea kumchagua raisi wetu atakaye tuongoza kwa kipindi kingine, tunahimizwa kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili tuweze kupata kitambulisho kitakachotupatia fursa ya kupiga kura mnamo October mwaka huu. Tambua kuwa kupiga kura ni muhimu kwa faida yako na Taifa kwa ujumla. Kumbuka kuwa kitambulisho cha mpiga kura ni hazina yako, kwani utaweza kukitumia katika shughuli mbalimbali pale utakapotakiwa kutoa kitambulisho. Aidha kwa namna moja au nyingine chaweza kukutambulisha wewe ni raia wawapi. Watanzania wenzangu tusipoteze fursa hii ya kupata kitambulisho. Tujitokeze kwa wingi katika kupata vitambulisho ili tuweze kupiga kura mwezi October. Kumbuka chagua kiongozi bora mwenye dira na dhamira ya dhati kwa watanzania wote wa hali zote. JITOKEZE UPATE KITAMBULISHO CHAKO. USIPUUZIE NI KWA FAIDA YAKO.